Ads 468x60px

Sunday, April 13, 2014

Breaking: Bomu La Kutupa Lalipuka Arusha night park Mianzini Usiku Huu!

 
Inasemekana kitu kinachoaminika kuwa bomu la mkono kimetupwa kwenye Bar ya Arusha night park Mianzini wakati watu wakitazama mpira.

Watu wa maeneo ya karibu kama Soweto walisikia mlio mkubwa ulioambatana na taarifa ambazo bado hazijathibitishwa kwamba vimetokea vifo na wengine wamejeruhiwa kwa kukatika mikono na miguu.

Usiku wa April 13 2014 kwenye baa iitwayo ‘Arusha night park’ iliyopo Mianzini Arusha ambayo siku zote ni miongoni mwa sehemu zinazokua na mkusanyiko wa watu wengi kuanzia jioni, limerushwa bomu wakati watu mbalimbali wakitazama mpira.
Blog hii imepata nafasi ya kuongea na mkuu wa mkoa wa Arusha ambae ni kiongozi 
wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ambae amethibitisha kwamba ni 


watu 15 wamejeruhiwa kwenye mlipuko huo.
Anasema
 wote wamepelekwa hospitali ambapo uchunguzi wa awali umeonyesha bomu 
hilo ni la kutengenezwa kwa mkono na mpaka sasa hajajulikana 

alietekeleza shambulio hilo.


Kwenye sentensi nyingine pia amesema hakuna aliepoteza maisha kwenye shambulio hilo ambalo uchunguzi wa awali umeshatoka, ila baadae itatoka taarifa rasmi pale uchunguzi kamili utakapokamilika.

0 comments:

Post a Comment