Dakika
90 za mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara katika viwanja vitatu tofauti
zimemalizika huku Azam wakijihakikishia pointi tatu muhimu za
kujitangazia ubingwa wa Ligi msimu huu wa 2014, kwa kuwabanjua Mbeya
City mabao 2-1. na kufikisha jumla ya Pointi 59. Katika uwanja wa Sheikh
Amri Abeid jijini Arusha, Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi
ya JKT Orjolo na kufikisha jumla ya Pointi, 55. na Mbeya City wanabaki
katika nafasi ya tatu. Na katika Uwanja wa Taifa Ashant United
wameifunga Simba bao 1-0.
Kutoka
Mbeya, John Boko, anaipatia Azam bao la pili, na sasa Mbeya City 1 Azam
2. Kutoka Jijini Arusha Yanga 2 Orjolo 1, mabao ya Yanga yamefungwa na
Zahri na Ngasa.
NA SUFIANI MAFOTO








0 comments:
Post a Comment