Ads 468x60px

Sunday, April 13, 2014

Hatari ya daraja Mbagala lililonyima magari kwenda mikoa ya kusini na ya kuingia Dar

Mvua zinazoendelea kunyesha mikoa tofauti Tanzania bado zimeendelea kuleta madhara ambapo pamoja na taarifa ya Watanzania kadhaa kukosa makazi na wengine kupoteza maisha bado barabara na madaraja vimezidi kubomoka.
Hizi picha ni za daraja la mto Mzinga ambalo ndilo linalounganisha Dar na mikoa ya kusini limeanza kumeguka kufuatia mvua iliyonyesha na inayoendelea kunyesha ambapo sasa Wasafiri wa kwenda Nachingwea, Masasi, Tunduru, Mtwara, Lindi na maeneo jirani wamekwama.
Baadhi ya kampuni ambazo zinamiliki zaidi ya mabasi manne, zimekua zikifaulisha wasafiri toka kwenye mabasi yaliyokwama upande wa Mtwara kuingia kwenye basi lililo upande wa Dar na wa Dar kuingia basi la Mtwara ili safari ziendelee.

0 comments:

Post a Comment