Makamu
wa Rais Dk. Mohamed Gharibu Bilali akikabidhi tuzo ya Ushindi wa kwanza
Kitaifa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kwa kuibuka
washindi wa jumla katika Kundi la Taasisi za Utafiti na Mafunzo.
Anaepokea ni Mkurugenzi Masoko, Mipango na Maendeleo, wa VETA - Tanzania, Enock Kibendera
Featured Posts Coolbthemes
Saturday, August 9, 2014
WAZIRI WA UJENZI DK. MAGUFULI AIFAGILIA NSSF UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI
WAZIRI
wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ameusifu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
kwa kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa daraja la Kigamboni.
Ujenzi
wa daraja hilo umekamilika kwa asilimia 60 ambapo mpaka sasa NSSF
imetoa sh. bilioni 117 kati ya Bilioni 214 zitakazokamilisha ujenzi wa
daraja hilo.
Akizungumza
leo jijini Dar es salaam, alipotembelea daraja kuona namna ujenzi
unavyoendelea, Dk. Magufuli alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo umekutana
na changamoto nyingi ikiwemo kina kilichokuwa katikati ya bahari
kupoteza malighafi ya ujenzi ambapo wahandisi waliamu kufanya utafiti.
Alisema kuwa juhudi za NSSF katika kufadhili mradi huo umewezesha changamoto zilizokuwa zikiukabili maradi huo kufanyiwa kazi.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa NSSF, Ludovick Mrosso, alisema kuwa mradi huo
unatarajiwa kukamilika Julai, 2015 ambapo katika daraja zitakuwa
barabara sita za magari, mbili za wapita kwa miguu.
Maradi huo unajengwa kwa kushirikisha Wizara ya Ujenzi, NSSF na Tanroads.
AJALI ENEO LA AFRIKANA, MBEZI BEACH MCHANA WA LEO
Gari aina ya Nissan Hard Body yenye Namba za Usajili T 524 ALW likiwa limetupwa mtaroni na trela la lori (halipo pichani) ambalo
lililigonga gari hilo na kutumbukia mtaroni eneo la Afrikana Mbezi
Beach Mchana wa leo. Katika Ajali hiyo iliyohusisha Lori na gari aina ya
Nissan Hard Body hakuna mtu yoyote aliyepoteza Maisha
Wananchi
wakisaidia Kulifunga minyororo gari aina ya Nissan Hard Body ambayo
imetumbukia mtaroni mara baada ya Kugongwa na trela la lori (halipo pichani) mchana wa leo katika Eneo la Mbezi Afrikana
Wananchi
wakisaidia kuligeuza gari ndogo aina ya Nissan Hard Body iliyotumbukia
mtaroni eneo la Afrikana Mbezi Beach mara baada ya Kugongwa na trela la
lori (halipo pichani) mchana wa leo, katika ajali hiyo hakuna
aliyepoteza maisha. Picha zote na Josephat Lukaza Wa Lukaza Blog
MAONYESHO YA NANENANE NGONGO MKOANI LINDI
MCHUMI MKUU KUTOKA WIZARA YA FEDHA ADAM MSUMULE AKITOA MAELEZO KWA NAIBU KATIBU MKUU,
WIZARA YA NISHATI NA MADINI, INJINIA NGOSI MWIHAVA KATIKA VIWANJA VYA
MAONYESHO YA NANENANE NGONGO MKOANI
LINDI.
WANANCHI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI JANET EZEKIEL, AFISA
UHUSIANO WA PPF KATIKA MAONYESHO YA
KITAIFA YA NANENANE YANAYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA NGONGO MKOANI LINDI.
AFISA MAWASILIANO NA
MASOKO RAHMA NGASSA [KULIA] NA
AFISA MFAWIDHI MKUU PSPF, MTWARA OMARY
KALILO [ KUSHOTO] WAKISHUHUDIA MKUU WA
WILAYA YA LINDI MJINI DKT. NASSORO ALI HAMIDI AKISAINI KITABU CHA WAGENI
ALIPOTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA KATIKA VIWANJA VYA NANENANE NGONGO MJINI
LINDI
ERICK MHOKOLE MKUTUBI
KUTOKA CHUO CHA MIPANGO DODOMA AKITOA UFAFANUZI KWA WANANCHI WALIOTEMBELEA
BANDA LA WIZARA YA FEDHA MJINI LINDI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE KITAIFA
YANAYOENDELEA KATIKA VIWANJA VYA NGONGO.
NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI INJINIA NGOSI MWIHAVA AKISAINI KITABU CHA
WAGENI KATIKA BANDA LA UTT ASSET MANAGEMENT , KULIA AFISA MASOKO NA UHUSIANO
RAHIM MWANGA AKITOA MAELEZO KWA WAGENI.

MENEJA WA MKOA WA
LINDI WA WAKALA WA HUDUMA YA UNUNUZI SERIKALINI [GPSA] , MWAKISELU MWAMBANGE
AKITOA MAELEZO KWA MSHIRIKI ALIYETEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA KATIKA
MAONYESHO YA KITAIFA YA NANENANE YANAYOFANYIKA NGONGO MKOANI LINDI.
MENEJA WA PPF KANDA YA KUSINI, ANTHONY NDADAVALA AKITOA MAELEZO KWA WANACHAMA WA PPF
WALIOTEMBELEA BANDA LA WIZARA YA FEDHA KATIKA MAONYESHO YA NANENANE
YANAYOFANYIKA NGONGO MKOANI LINDI.
Thursday, July 17, 2014
MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2014 YATOKA
Matokeo ya mtihani wa kidato cha 6 yaliyofanyika tarehe Mei 5 – 21, yametoka.
Jumla ya watahiniwa 38,905 sawa na asilimia 95.98 ya watahiniwa
waliofanya mtihani kidato cha 6 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni
12,080 na wavulana waliofaulu ni 26,825.
Watahiniwa waliopata division IV ni 4,420 sawa na asilimia 12.54
Watahiniwa waliopata zero (0) ni 612 sawa na asilimia 1.74.
SHULE 10 ZILIZOONGOZA
1. Igowole
2. Feza Boys
3. Kisimiri
4. Iwawa
5. Kibaha
6. Marian Girls
7. Nangwa
8. Uwata
9. Kibondo
10. Kawawa
SHULE 10 ZA MWISHO
1. Ben Bella
2. Fidel Castro
3. Tambaza
4. MuhezaHigh School
5. Mazizini
6. Mtwara Technical
7. Iyunga technical
8. Al- falaah Muslim
9. Kaliua
10. Osward Mang'ombe
Kuona matokeo pitia hapa: http://www.necta.go.tz/matokeo2014/ACSEE.htm
MATOKEO
KIDATO CHA 6: 95.98% wafaulu kidato cha 6 kutoka 87.9% mwaka jana.
Tambaza ndani ya shule 10 za mwisho,
K/Katibu Mtendaji Necta
C. Msonde
atangaza leo.
K/Katibu Mtendaji Necta
C. Msonde
atangaza leo.
Feza Boys and Girls Secondary Schools emerge Top in Dar es salaam
The National
Examination Council of Tanzania ( NECTA) has
released the Form Six National Examination results for 2014 indicating
better performance over last year’s record.
The results from the
examination sat on may this year showed Feza Boys High school topping the lists of
schools in terms of best performance in Daresalaam and ranked 2nd nationalwise followed
by the sister school Feza girls High school which became 2nd in Daresalaam
and 12th nationalwise.
A total of 60 candidates sat for the exam where
36 got division I, 18 students got division II and 6 students got division III
which made the school 2nd nationalwise, and Feza girls had 41
candidates where 19 students got division I, 13 division II, and 9 division
III’s .
The results further showed
that Feza boys High school as the overall best school in science subjects as it
topped chemistry, biology, history and Economics nationalwise.
The 2 students from
Feza boys high school, Innocent Sabas Yusuf (3rd) and Ramadhan Msangi(10th), managed to become
among the top ten best students in Tanzania.
Since its commencement in the year 1998, Feza
Schools have been pioneering provision of quality education to the Tanzanian
Youth. From nursery, primary, secondary to high level education the school has
established spacious compounds with home touch, teaching by Tanzanian
curriculum for both boys and girls.
Feza Schools have even recently opened an
International school for both boys and girls, following the Cambridge
Curriculum to suit more needs of the Tanzanians seeking for alternative
education systems.
TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014
Jumla ya watahiniwa 38,905 sawa na asilimia 95.98 ya watahiniwa waliofanya mtihani kidato cha 6 wamefaulu.
Wasichana waliofaulu ni 12,080 na wavulana waliofaulu ni 26,825
Watahiniwa waliopata division IV ni 4,420 sawa na asilimia
12.54
Watahiniwa waliopata zero (0) ni 612 sawa na asilimia 1.74.
WAFUASI WA CCM,CHADEMA NUSURA WAZICHAPE KAVU KAVU MKUTANO WA NAIBU WAZIRI WA MAJI, AMOS MAKALLA
Mbunge
wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan wa CCM (kulia), akiamulia ugomvi wa
Diwani wa Kimara, Pascal Manota wa Chadema (kushoto) na Mwenyekiti wa
CCM, Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge waliotaka kuzichapa ulipotokea
mzozo katika mkutano wa hadhara wa Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla
katika Uwanja wa Shule ya Mavurunza, Kata ya Salanga, Jimbo la Ubungo,
Dar es Salaam jana.
TIMU YA AFRIKA YA KUSINI YAWASILI NCHINI KUIVAA SERENGETI BOYS JULAI 18
Kikosi cha Serengeti Boys.
Afrika
Kusini (Amajimbos) imewasili nchini kuikabili Tanzania (Serengeti Boys)
katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa
vijana wenye umri chini ya miaka 17 itakayochezwa keshokutwa (Julai 18
mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Timu
hiyo yenye msafara wa watu 37 ilitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) jana usiku (Julai 15 mwaka huu) na imefikia hoteli
ya Sapphire. Amajimbos itafanya mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja
wa Azam Complex.
Waamuzi
watakaochezesha mechi hiyo kutoka Shelisheli wakiongozwa na Allister
Barra tayari wamewasili nchini. Kamishna wa mechi hiyo ni Andriamiasasoa
Doda Nirimboavonjy kutoka Madagascar.
Makocha
wa timu za Seregenti Boys na Amajimbos pamoja na manahodha wao watakuwa
na mkutano na waandishi wa habari kesho (Julai 17 mwaka huu) saa 5
asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 2,000. Tiketi zitauzwa uwanjani katika magari maalumu siku ya mechi.
NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA HABARI,VIJANA,NA MICHEZO AZINDUA RASMI KITABU CHA "HISTORIA YA KLABU YA SIMBA"KILICHOANDIKWA NA MWINA KADUGUDA
Mwina
Kaduguda Mtunzi wa kitabu cha "HISTORIA YA SIMBA" akielezea kwa kina
Magumu gani amepitia wakati anaanza kuandaa kitabu hicho,Wa kwanza
Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Mheshimiwa Juma Nkamia na Katikati ni Mkurugenzi wa Mkuki na
Nyota Bwana Mkuki Bgoya ambao ndio wachapishaji wa kitabu
hicho.Akielezea kwa ufupi Mwina Kaduguda amesema kwamba Dhumuni kubwa la
Kutunga kitabu hicho ni kutaka kutunza historia ya soka ya Timu hiyo
isipoteee ili iweze kusomwa kizazi na kizazi.
Msaada tutani: mtoto aibwa changanyikeni leo, ataemuona atoe taarifa polisi

ATAKAEMUONA NNAOMBA ATUSAIDIE KUTOA TAARIFA KITUO CHOCHOTE CHA POLICE. AMEIBIWA NA MKAKA KANYOA PANK.
Please upatapo ujumbe huu mfowardie na mwenzako
Saturday, July 12, 2014
KONGAMANO LA NNE LA MAKATIBU MUHTASI TANZANIA (TAPSEA) LAFUNGULIWA LEO JIJINI MWANZA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk.
Mary Nagu akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu
Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Nagu katika hotuba
yake,amesema atawasimamia Makatibu hao na kuhakikisha wanaanzisha Benki
yao ambayo itawawezesha kuweka abiba zao na kukopeshana pia.
Mgeni
Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania,Naibu Waziri wa
Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake katika ufunguzi
wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013
jijini Mwanza.Mh. Kairuki amewahimiza Makatibu Muhtasi hao kuhakikisha
wanaudumisha na kuulinda umoja walionao,kwani umoja ndio msingi wa
maendeo.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu pamoja na Mgeni Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki wakati wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.
Picha ya pamoja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu akifurahi jambo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki mara baada ya ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda. Picha na Othman MichuzDAKTARI FEKI MWINGINE ADAKWA HOSPITALI YA RUFAA MOROGORO
Askari Polisi wakimtoa nje daktari feki, Karume Habibu (22) kutoka kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako alihojiwa kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano zaidi.
UNATAKA KUPUNGUA UZITO CLEAN 9 NDIO SULUHISHO LAKO!!

CLEAN 9 ni nini na ina nini??
Ina mchanganyiko wa bidhaa nne (Alovera Gel chupa 3, Ultra Lite, Bee pollen na Garcinia. Pia ina tape measure pamoja na chupa ya kupimia)
Ina kitabu cha muongozo wa jinsi ya kutumia.
CLEAN 9 ni muhimu katika kupunguza mwili kwasababu inafanya kazi ya kusaidia mfumo wako wa mmeng'enyo wa chakula,kuondoa sumu mwilini, kuondoa mafuta yaliyozidi mwilini na kukupa mfumo bora wa ulaji chakula.
Matumizi yake ni rahisi sana. Tumia bidhaa kwa usahihi kisha utahitaji kufanya mazoezi walau dakika 20 (kutembea,kuruka kamba,kukimbia au gym ukipenda), Kunywa maji ya kutosha angalau lita tatu kwa siku punguza au acha kabisa ulaji wa vyakula vyenye sukari,wanga na mafuta.
Unatumia kwa siku tisa na itakusaidia kupungua kilo 3 mpaka 8 na kupungua zaidi utatumia Nutri lean ambayo ina bidhaa za mwezi mzima na una uwezo wa kupungua kilo 10 mpaka 15...
Wasiliana nasi kwa mawasiliano hapo juu
Ina mchanganyiko wa bidhaa nne (Alovera Gel chupa 3, Ultra Lite, Bee pollen na Garcinia. Pia ina tape measure pamoja na chupa ya kupimia)
Ina kitabu cha muongozo wa jinsi ya kutumia.
CLEAN 9 ni muhimu katika kupunguza mwili kwasababu inafanya kazi ya kusaidia mfumo wako wa mmeng'enyo wa chakula,kuondoa sumu mwilini, kuondoa mafuta yaliyozidi mwilini na kukupa mfumo bora wa ulaji chakula.
Matumizi yake ni rahisi sana. Tumia bidhaa kwa usahihi kisha utahitaji kufanya mazoezi walau dakika 20 (kutembea,kuruka kamba,kukimbia au gym ukipenda), Kunywa maji ya kutosha angalau lita tatu kwa siku punguza au acha kabisa ulaji wa vyakula vyenye sukari,wanga na mafuta.
Unatumia kwa siku tisa na itakusaidia kupungua kilo 3 mpaka 8 na kupungua zaidi utatumia Nutri lean ambayo ina bidhaa za mwezi mzima na una uwezo wa kupungua kilo 10 mpaka 15...
Wasiliana nasi kwa mawasiliano hapo juu
NYUSI AJINADI KWA WANAMSUMBIJI WANAISHI ZANZIBAR

Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akipokea zawadi kutoka kwa Jumuiya ya watu wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar.
Tuesday, June 24, 2014
RAIS KIKWETE KIKWETE AWAAPISHA BALOZI NA WAJUMBE WA TUME YA OPERESHENI TOKOMEZA IKULU DAR
Balozi Joseph Edward Sokoine akila kiapo,kupokea miongozo ya kazi na kupongezwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amemwapisha balozi mmoja pamoja na
wajumbe wanne wa Tume ya Operesheni Tokomeza katika hafla fupi
iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.
Balozi
aliyeapishwa ni Joseph Edward Sokoine ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya
Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.Wajumbe walioapishwa nia pamoja na Mwenyekiti wa tume hiyo
Jaji Mstaafu Hamisi Amiri Msumi, Jaji Mstaafu Steven Ernest Ihema,Jaji
Mstaafu Vincent Damian Lyimo pamoja na katibu wa tume hiyo Bwana
Frederick Kapela.
Wajumbe
wa Tume ya operesheni Tokomeza wakiwakatika picha ya pamoja na Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal (Wanne
Kushoto) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kulia)
wajumbe hao kutoka kushoto ni Katibu wa Tume hiyo Bwana Frederick Kapela
Manyanda, Jaji Mstaafu Vincent Damian Lyimo(wapili kushoto), Jaji
mstaafu Hamisi Amiri Msumi(Watatu kushoto), na Jaji Mstaafu Steven
Ernest Ihema (kulia),Wasita kushoto ni Balozi Joseph Edward Sokoine.
Picha ya pamoja na Balozi na Wajumbe wa Operesheni tokomeza. Picha na Freddy Maro
Friday, June 13, 2014
SOKO LA ILALA MCHIKICHINI JIJINI DAR LILIVYOTEKETEA KWA MOTO LEO
Sehemu
ya wafanyakazi wa Kikosi zimamoto wakiendelea na zoezi la kuzima moto
ulioteketeza kabisa Soko la Ilala Mchikichini Jijini Dar es salaam
leo.Moto huo ulianza majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo na
kuteketeza kila kilichokuwepo katika eneo la soko hilo. Chanzo cha
kutokea kwa moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa.Picha zote na Othman
Michuzi.
Subscribe to:
Comments (Atom)





















