
Mabaharia wa kikosi cha jeshi la baharini la Australia wamekamata magunia 46
ya dawa za kulevya aina ya heroine zenye thamani ya dola milioni 290, kwenye
boti moja katika fukwe ya bahari nchini Kenya.
Kwa mujibu Shirika la Utangazaji la Australia dawa hizo za kulevya zilikuwa
zimefichwa chini ya mifuko ya saruji.
Mnamo mwaka 2004, cocaine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.4 ilikamatwa
Nairobi na Malindi Kenya ambayo inasemekana kuwa ni shehena kubwa ya dawa za kulevya
kuwahi kukamatwa barani Afrika.








0 comments:
Post a Comment