Ads 468x60px

Friday, April 25, 2014

KIJANA MLEVI ATISHIA KUITEKA NDEGE YA AUSTRALIA IKIWA ANGANI

 Ndege ya Australia iliyokuwa na abiria 137 na wahudumu 6 ikitokea Brisbane Australia, imetua katika uwanja wa ndege wa Bali nchini Indonesia na uwanja huo kulazimika kufungwa kwa muda baada ya mmoja wa abiria aliyekuwa ndani ya ndege hiyo kujaribu kutaka kuiteka ndege hiyo. 


Kijana huyo ametajwa kwa jina la Matt Christopher mwenye miaka 28 ni raia wa Australia na alikuwa amelewa wakati akifanya kitendo hicho. 


Awali rubani wa ndege hiyo aliwasiliana na mamlaka husika katika uwanja wa Bali na kuwajulisha juu ya tukio la kutaka kutekwa kwa ndege hiyo

 Ndege hiyo, Boeing 737-800 baada ya kutua katika uwanja wa Bali ilikuta ulinzi mkali umesha imarishwa wa vikosi vya kijeshi, na abiria wote wameripotiwa kuwa salama japo walipatwa na mshituko wa tukio hilo.

0 comments:

Post a Comment