Ads 468x60px

Saturday, May 10, 2014

Tanzia: Balozi wa Malawi nchini Tanzania afariki ghafla

Balozi wa malawi hapa Tanzania Flossy Gomile-Chidyaonga amefariki dunia ghafla na Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Malawi Bi Joyce Banda. 

Balozi huyo amefariki jana Ijumaa.

Balozi wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Flossy Gomile-Chidyaonga (pichani) amefariki dunia jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.

“Ni kwa masikitiko makubwa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (ya Malawi) unauarifu umma kufariki dunia kwa Balozi Flossy
Gomile-Chidyaonga baada ya kuugua kwa muda mfupi jijini Dar es salaam mchana huu”, imesema taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara hiyo Quent Kalichero.

“Tangu mwaka 2006 Marehemu Bi Flossy Gomile-Chidyaonga alikuwa
Naibu Balozi wa Malawi London kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania mnamo Septemba mwaka 2011”, imesema taarifa hiyo na kuongezea kuwa taratibu za mazishi zitatangazwa baada ya taratibu kukamilika.

CHANZO: BOFYA HAPA

0 comments:

Post a Comment