Mfungaji
bora wa Timu ya Watoto wa Mitaani kutoka Mwanza Tanzania, (TSC)ambayo
iliibuka mshindi katika mashindano Kombe la Dunia la Watoto hao
yaliyofanyika Brazil, mwaka huu Frank William ameishauri , Serikali na
jamii kuwasaidia watoto wa mitaani ili kuweza kukuza vipaji vyao.
Kauli
hiyo ilitolewa leo mjini Dodoma na William wakati walipolitembelea
Bunge Maalum la Katiba Mjini Dodoma , wakiwa na viongozi wao ,ambapo
walipata nafasi ya kuzungumza na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo, Dk. Fenella Mukangara pamoja na Naibu wake Juma Nkamia.
Alisema siri
ya ushindi wetu ni ushirikiano na kujituma, tukilikwenda kuwakilisha
watoto wengine wa mitaani. Hivyo aliomba jamii kuwasaidia watoto wengi
wa mitaani ambao hawana uwezo wa kupata elimu lakini wana vipaji
mbalimbali ili waweze kuvikuza.
Kwa
upande wake kipa bora wa timu hiyo, Emmanue Amos, alishauri Serikal
iweze kuwasaidia ili waweze kushiriki katika mashindano ya mwaka 2018
ya kombe hilo.
Mchezaji
mwingine wa timu hiyo ,Denis David aishauri jamii isiwadharau kwa kuwa
ni watoto wa mitaani kwani wanavipaji wakipata watu wa kuwasaidia,
hivyo aliitaka iwekeze katika soka la vijana kwa sababu baada ya
miaka 20 ijayo mchezaji bora anapatikana kwa njia hiyo.
Aliwaomba wajumbe wa Bunge hilo ,kuwasaidia ili waweze kuvikuza vipaji vyao.
Naye
Kocha wa timu hiyo,Suileiman Jabir alisema
wadau mbalimbali kuwasaidia na kuwaendeleza watoto hao I, ambao ni
wengi ambao wanaweza kuwa na vipaji vya sanaa na utamaduni.
Akizungumzia
kuhusu mafanikio ya ushindi huo, ni kuwa na mpango wa kutafuta vijana
wenye vipaji ambapo wanaviendeleza na kuvikuza kwa kufanya maandalizi
ya kiutalaamu na kiufundi.


Jabir aliongeza kuwa waliwandaa kisaikolojia ili waweze kushinda katika mashindano hayo ya kimataifa.
Aliwataka wajumbe wa Bunge hilo,
kuhakikisha was aula la watoto hao, linapewa kipaumbele na kuweka
sheria itakayowadhibiti wakina baba wanatekeleza watoto,huku akiisa
jamii kuwasaidia watoto pale wazazi au walezi wanapofariki dunia.
Rais
wa timu hiyo, Altaf Hirani aliiomba Serikali kuweza kuwasaidia kupata
kiwanja cha michezo kwa ajili ya watoto jijini Mwanza au
kwenye maeneo mengine ya nchi.














0 comments:
Post a Comment