Viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick na kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova walianguka na Helikopta hii asubuhi ya April 13 2014 kwenye uwanja wa ndege Dar.
Hitilafu ilisababisha helikopta kuanguka wakati ikipaa kuwapeleka kwenye maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo hata hivyo walinusurika kifo isipokua majeraha madogomadogo tu.

Kama unataka ripoti kama hizi zisikupite, jiunge na familia ya millardayo.com kupitia twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la MillardAyo ili niwe nakutumia kila ripoti inayonifikia.


Taarifa iliyoifikia millardayo.com
kutoka kwa mmoja wa Waliokuwemo kwenye Helikopta hii ya jeshi inasema
wakati inapaa kwenye umbali wa kama futi tano hivi kutoka uwanja wa
ndege Dar es salaam, ilizidiwa na upepo ulioirudisha nyuma na kuangukia
paa kabla ya kutua chini.
Kilichofanyika ni watu waliokuwemo kutoka nje harakaharaka kisha
aliekua akiiendesha kufungua tenki la mafuta na kumwaga mafuta yote
alafu baada ya muda mfupi vikosi vya zimamoto vikaanza kuipiga maji
helikopta hiyo ili kuepusha mlipuko.
Unaambiwa kama ingekua ni majira ya moto, helikopta hii ambayo ilikua
inawapeleka kutazama maafuriko yaliyookana na mvua Dar es salaam
ingeweza kuwa kwenye hatari zaidi ya kulipuka.
Ndani
ya Helikopta walikuwepo watu mbalimbali akiwemo Makamu wa rais Dr.
Bilal, Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova na
mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Mecky Sadick.
Kama unahitaji matukio kama haya yasikupite, jiunge na mimi kwenye twitter instagram na facebook kwa jina hilohilo la MillardAyo ili niwe nakutumia kila ripoti inayonifikia usiku au mchana.
Picha zote mbili kutoka http://nasmamafoto.blogspot.com/









0 comments:
Post a Comment