Mamilioni
ya watu wengine duniani wameangalia kupitia runinga tukio hilo la
viongozi wa zamani wa kanisa katoliki wakipewa utakatifu.
Vatican
ilitarajia watu milioni 1 kukusanyika kwenye kanisa hilo pamoja na
barabara za kuelekea kwenye kanisa la St. Peter’s Basilica. Sherehe
hizo zimehudhuriwa na makadinali 150, maaskofu 1,000 na mapadre 6,000.
Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 100 nao wamehudhuria wakiwemo marais
24.
Papa
Emeritus Benedict XVI, aliyejiuzulu mwaka jana kwa sababu za kiafya
alialikwa na Papa Francis lakini hakuwepo kwenye madhabahu
Rais Robert Mugabe na familia yake
Tukio hilo ni kubwa zaidi jijini Vatican tangu kuchaguliwa kwa Papa Francis mwaka jana.
Hizi ni baadhi ya picha.

Waumini wa kanisa katoliki wakifuatilia sherehe za kutangazwa watakatifu mapapa John XXIII na John Paul II
Mapapa wa zamani, John XXIII na John Paul II wametangazwa watakatifu
Jumapili hii na Papa Francis hafla iliyoshuhudiwa na umati mkubwa wa
waumini wa kanisa katoliki kwenye viwanja vya St. Peter’s Square, jijini
Vatican.















0 comments:
Post a Comment