Ads 468x60px

Wednesday, April 30, 2014

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Richard Sezibera akimkaribisha Rais  Dkt Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya hiyo unaofanyika leo.
 Rais  Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha(AICC) kwenye mkutano wa 12 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mjini Arusha.Rais Kenyatta ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya wnanachama watano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakijadiliana jambo kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa siku moja wa  wakuu wa nchi za  Jumuiya ya Afrika Masharariki uliofanyika mjini Arusha leo. Picha na Freddy Maro.

MTOTO WA MAAJABU ALIYEZALIWA CAMEROOM


Mtoto wa majabu azaliwa nchini cameroon, amezaliwa akiwa na jicho moja ndani ya hilo jocho kuna macho mawili, pia amezaliwa akiwa hana pua wala mdomo na amezaliwa na jinisia mbili.

CHANZO: BOFYA HAPA

SAFISHA JIJI YAENDELEA LEO KARIAKOO JIJINI DAR

Tingatinga la Manispaa ya Ilala likibomoa vibanda vilivyojengwa maeneo yasiyoruhusiwa Kariakoo katika operesheni safisha jiji iliyofanyika Dar es Salaam, mitaa ya Aggrey na Livingstone.
Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiimarisha ulinzi wakati wa oparesheni hiyo.

PSPF WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA USALAMA NA AFYA DUNIANI KWA WAFANYAKAZI, MNAZI MMOJA DAR

Ofisa muendeshaji wa Mfukowa pesheni wa mashirika ya umma PSPF, Bw, Hadji Jamadary kushoto akimwelekeza kujaza fomu Shabani Maganga wakati wa mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaamAfisa muendeshaji wa mfuko wa pesheni wa mashirika ya uma PSPF Bw, Lule Kasembwe kushoto akitoa maelekezo kwa wazee waliojitokezaOfisa muendeshaji wa PSPF Hadji Jamadary kushoto akiwapatia mahelezo ya jinsi ya kujiunga na PSPF wakati wa mahadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Dar es salaam.

CHEKI HAPA VIDEO YA BAYERN MUNICH ILIVYOKUBALI KICHAPO CHA MABAO 4-0 KUTOKA KWA REAL MADRID NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA

MAGAZETI YA LEO JUMATANO

Tuesday, April 29, 2014

MAGAZETINI JUMANNE YA LEO

001_90921.jpg

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO ZAFANYIKA PARIS UFARANSA

Watanzania waishio nchini Ufaransa walikutana Jumamosi mchana tarehe 26 Aprili nyumbani kwa Balozi wa Tanzania mjini Paris ili kusherehekea miaka 50 ya muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika.
Balozi wa Tanzania Nchini Ufaranza,Mh. Begum Karim Taj akipokea keki maalum kwa ajili ya sherehe hizo za Muungano wa Tanzania katika hafla iliyofanyika nyumbani kwa Balozi,Mjini Paris Ufaransa.
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa akiwa na watoto mjini Paris.
Mh. Balozi Begum Taj akiwa na baadhi ya watanzania waishio nchini Ufaranza.
Kutoka kushoto: Ndg John Kimaro (Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale), Mh Begum Taj (Balozi wa Tanzania) na Rainfrida Kapela (Mhifadhi Mkuu wa Mambokale Bagamoyo).
Mh Begum Karim Taj akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Watanzania Ufaransa Mh Delly Makombe.
Ndugu Mohammed Sheya akiimba wimbo wa Taifa.
Mama Delly , Mh Balozi Tah na Mama Matari wakikata keki.
Burudani ya uhakika ikiendelea.
Ndg John Kimaro (katikati) akiongea na wageni wakati wa sherehe za Muungano
Mama Rainfrida Kapela Mhifadhi Mkuu wa Mambo ya Kale Bagamoyo
Vyakula mbalimbali katika kuenzi miaka 50 ya muungano.
Baadaye ikawa kazi ya kufungua 'champaign' kuenzi sherehe za Muungano.Picha na Mdau Simplish Lakshi.

Monday, April 28, 2014

Licha ya Serikali kupiga marufuku uuzwaji wa mazao ya wakulima bila kutumia vipimo sahihi bado tatizo hilo limeendelea kuota mizizi katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya.


PAPA FRANCIS AWATANGAZA MAPAPA JOHN XXIII NA JOHN PAUL II WATAKATIFU

 Mamilioni ya watu wengine duniani wameangalia kupitia runinga tukio hilo la viongozi wa zamani wa kanisa katoliki wakipewa utakatifu.
Vatican ilitarajia watu milioni 1 kukusanyika kwenye kanisa hilo pamoja na barabara za kuelekea kwenye kanisa la St. Peter’s Basilica. Sherehe hizo zimehudhuriwa na makadinali 150, maaskofu 1,000 na mapadre 6,000. Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 100 nao wamehudhuria wakiwemo marais 24. 

MAGAZETI YA LEO JUMATATU


RAIS KIKWETE AZINDUA RASMI KITUO CHA MAGONJWA YA MOYO CHA MUHIMBILI

Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongea na mmoja wa wagonjwa watoto waliofanyiwa upasuaji kwenye kituo kipya na cha kisasa cha Moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kukifungua rasmi leo.Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete na Makamu Mwenyekiti wa chama tawala cha China cha National People's Congress Mhe. Chen Changzhi wakipata maelezo ya utendaji wa mashine katika chumba cha wagonjwa mahututi  kwenye kituo kipya na cha kisasa cha Moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kukifungua rasmi leo Sunday, April 27, 2014.Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete akiongea na mmoja wa wagonjwa watoto waliofanyiwa upasuaji kwenye kituo kipya na cha kisasa cha Moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kukifungua rasmi leo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho kikwete na Makamu Mwenyekiti wa chama tawala cha China cha National People's Congress Mhe. Chen Changzhi (kushoto) wakioneshwa moja ya vifaa vya kisasa vya kuchunguzia maradhi kwenye kituo kipya na cha kisasa cha Moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kukifungua rasmi leo.

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA ZILIVYOFANA WASHINGTON DC

Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Watanzania hapa Washington DC kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano.

NGORONGORO HEROES YAWAGALAGAZA VIJANA WENZAO WA KENYA KWA MIKWAJU YA PENATI 4-3


Mshambuliaji wa Ngorongoro, Ally Bilal (kulia) akichuana na beki wa Kenya, Geofrey Shivekwa, wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za michuano ya Kombe la Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, zinazotegemea kufanyika mwakani nchini Senegal. 

Katika mchezo huo Ngorongoro Heroes imewaondosha mashindanoni majirani zao wakenya kwa mikwaju ya penati, ambapo dakika 90 zilimalizika kwa kutoka suluhu na kuamuriwa kupigwa mikwaju ya penati kutokana na kwamba katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Kenya timu hizo zilitoka sare ya 0-0. Kenya wameondoshwa kwenye michuano hiyo kwa jumla ya penati 4-3 na kusonga mbele.

Iddi Suleiman  wa Ngorongoro (kulia) akichanja mbuga.

Wachezaji wa Ngorongoro, wakishangilia ushindi baada ya kushinda kwa penati na kusonga mbele.

Saturday, April 26, 2014

SHEREHE ZA MUUNGANO KITUO CHA GENEVA, SWITZERLAND ZAFANA

Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva,  Mhe.  Modest Mero, akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya watu wa  China-Geneva, Liu Jieyi katika tafrija maalum ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa ILO hii leo na kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali ikiwemo balozi huyo China UN mjini Geneva, Balozi wa Kenya, Balozi wa Afrika Kusini, Balozi wa Togo, Balozi wa Botswana, Balozi wa Cameroon, Balozi wa Rwanda, wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na Watanzania waishio Switzerland. Kushoto ni Mke wa balozi huyo Rose  Mero.

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO ZAFANA JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.

Friday, April 25, 2014

MAZUNGUMZO NJIA PEKEE YA KUREJESHA AMANI YA KUDUMU DARFUR - GEN-MELLA

Jenerali Mella, Kamanda wa Jeshi la UNAMID akibadilisha mawazo na Balozi Mwinyi, ambapo pamoja na mambo mengine, amesema wanajeshi kutoka JWTZ ambao ni sehemu ya UNAMID wameendelea kuonesha weledi na kujituma kwa hali ya juu katika eneo la ulinzi wa amani, ulinzi wa raia na usimamiaji wa misaada ya kibinadamu. Akasema kutokana na mapingano ya kikabili yanajitokeza mara kwa mara, na kuwa sehemu kubwa ya mapigano hayo yamekuwa yakitokea katika maeneo zilipo kambi za wanajeshi kutoka Tanzania, wanajeshi wetu wamejikuta wakilazimika kutoa huduma mbalimbali zikiwamo za kuwazalisha wanawake waja wazito. Utoaji wa huduma hiyo ya uzazi salama nje ya mamlaka yao imewafanya wazazi waliojifungua kuwapatia majina ya kitanzania watoto wao, kama shukrani yao kwa madaktari hao wa kitanzania kwa kuokoa maisha yao na ya watoto wao. Kushoto kwa Jenerali Mella, ni Luteni Kanali, Wilbert Ibuge, Mwambata Jeshi katika Uwakilishi wa Kudumu
Luteni Jenerali Paul Mella, Kamanda wa Jeshi la Mseto la Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika Darfur ( UNAMID) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ( hayupo pichani). Jenerali Mella alifika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kufuatia ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika Umoja wa Mataifa ambapo alikuwa na mazungumzo na Wakuu mbalimbali wa UN. Akielezea tathmini yake ya miezi nane kama Kamanda wa UNAMID Jenerali Mella anasema njia pekee ya kupatikana kwa amani ya kudumu katika jimbo la Darfur ni kwa pande zinazopingana kukaa katika meza ya mazungumzo na kumaliza tofauti zao.

Na Mwandishi Maalum

Kamanda wa Jeshi la Mseto la Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika Darfur ( UNAMID) Luteni Jenerali Paul Mella, amesema, mazungumzo yatakayozihusisha pande zote zinazopingana katika mgogoro na machafuko yanayoendelea katika Jimbo la Darfur ndiyo suluhu pekee inayoweza kurejesha hali ya Amani, usalama na utulivu katika jimbo hilo.

Jenerali Mella, ameyasema hayo wakati alipokuwa akibadilishana mawazo na Balozi Ramadhani Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakati Jenerali Mella alipoutembelea Uwakilishi wa Kudumu.

Kamanda wa Jeshi la UNAMID alikuwa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Viongozi mbalimbali wa Umoja wa Mataifa.

“Katika kipindi changu za miezi nane sasa kama kamanda wa UNAMID yapo mambo mengi ambayo nimejifunza zikiwamo pia changamoto mbalimbali katika eneo zima la ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darfur. Kubwa la msingi ambalo nimejifunza, ni kwamba, Amani ya kudumu haiwezi kurejea katika jimbo la Darfur kama pande zote zinazopingana hazitaweza kukaa katika meza moja na kufanya mazungumzo” anasema Jenerali Mella.

Na kuongeza “ kwa tathmini yangu , wanajeshi wanaounda UNAMID wapo pale kulinda Amani, kutoa ulinzi kwa wananchi na kusaidia usambazaji wa misaada ya kibinadamu. Lakini kwa kweli, hakuna Amani ya kulinda, kwa sababu moja kubwa, nayo ni kwamba pande zinazopingana hazijafikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kurejea katika meza ya mazungumzo.”

Akielezea zaidi tathmini yake katika kipindi hicho ya miezi nane ambapo anaongoza zaidi ya walinzi wa Amani (wanajeshi)14,379 wanaounda UNAMID. Jenerali Mella, anaeleza kwamba, tangu achukue uongozi huo, kumekuwapo na mabadiliko katika mwenendo mzima wa mapigano katika jimbo hilo.

“ Changamoto kubwa niliyokumbana nayo ni kuwa katika miezi hiyo nane ya uongozi wangu, mwenendo mzima wa machafuko au mapingano umebadilika na kujikita zaidi katika mapigano ya kikabila” anabainisha na kuongeza.

“Mapigano hayo ya kikabili na ambayo chimbuko lake ni kugombea raslimali zikiwamo dhahabu mafuta na malisho, yamepelekea kuwapo kwa wimbi kubwa la wakimbizi wa ndani.

Jenerali Mella anasema, sehemu kubwa ya mapingano hiyo baina ya makabila yalikuwa yanatokea karibu na maeneo zilipo kambi zetu kwa maana ya wanajeshi kutoka Jeshi la wananchi wa Tanzania ( JWTZ). Ninafarijika sana kueleza kwamba wanajeshi wetu wameonyesha weledi na uhodari wa hali ya juu kwanza kwa kutoa ulinzi kwa raia waliokuwa wakikimbia machafuko na pili kuwapatia misaada ya kibinadamu zikiwamo huduma za afya”.

“Ni katika kipindi hicho cha mapigano ambapo licha ya utoaji wa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi hao, walinzi wetu wa Amani ( JWTZ), walijikuta wakilazimika kutoa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito zaidi ya saba waliojifungua salama watoto wao katika kambi zetu”.

“ Huduma hii ya kuwasaidia akina mama wajawazito kujifungua salama watoto wao, kuliwafanya wazazi wale kuwapa watoto wao majina ya kitanzania kama shukrani yao kwa msaada na huduma nzuri waliyopatiwa na madaktari wa kitanzania katika kipindi hicho kigumu. Kuna watoto wenye majina ya kitanzania” anasema Jenerali Mella kwa furaha.

Kwa upande wake, Balozi Mwinyi ameshukuru Kamanda wa Jeshi la UNAMID kwa kutenga muda wake na kufika Uwakilishi wa Kudumu. Akashukuru pia kwa maelezo yake ya kina kuhusu hali ilivyo katika jimbo hilo la Darfur na mchango mzima wa walinzi wa Amani.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ina kikosi UNAMID kinacho kalia maeneo matatu ambayo ni Khor Abeche, Menawashe na Shangil Tobaya.

Tanzania inakuwa nchi ya tatu kongoza UNAMID , nchi nyingine ambazo zimewahi kuongoza ni Nigeria na Rwanda.

Kisa cha Mustapha kunyanyaswa na mkewe, unafahamu alichokuwa anakitaka?

joyce kiria

Je, umepata nafasi ya kufuatilia kisa hiki? Ni suala la kweli lililomkuta Mustapha ambaye analalamikia kunyanyaswa na mke wake. Joyce Kiria na Wanawake Live tulipata nafasi ya kufuatilia kwa undani suala hili na hapa, pata sehemu ya kwanza na ya pili ya mazungumzo kati ya Super Woman Joyce Kiria na Mustapha kisha na mke wake Mustapha kufahamu mustakabali mzima wa familia hii.

Je, baba Mustapha alipata alichokitaka? Ni nini hicho alichotaka? Tazama video hizi 3, na pia unaweza ukatembelea www.wanawakelivetv.com kwa ajili ya mengi zaidi.

Wasafirishaji na wauzaji dawa za kulevya siku zako zinahesabika – JK

FSA_8754
Rais Jakaya Kikwete akisalimia na Waziri wa Uchukuzi, Dkt Harrison Mwakyembe wakati  akiingia katika uwanja wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria jijini Dar es Salaam.

GEORGETOWN UNIVERSITY MAGAZINE TALKS ABOUT AFRICA AND MO DEWJI

DSC_0310
Mohammed Dewji (MP), CEO of Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL).

MAMA WANNE APELEKWA KATIKA KITUO MAALUMU NA WATOTO WAKE WAWILI WALIOBAKI KWA AJILI YA UANGALIZI.

Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Aisha Mtanda, alisema wameguswa na mazingira anayoishi mama huyo na kuamua kumpa uangalizi kwa miezi sita zaidi.

UNHWA ya Korea Kusini Kuisaidia NIMR katika Uguduzi wa Dawa kwa Kutumia Mimea

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Mtendaji Mkuu wa kampuni ya UNHWA ya Jamhuri ya Korea Kusini  Bw. Young Woo Jin na ujumbe wake na uongozi wa NIMR walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo